Search this site or the web

Site search Web search

KIDATO I KIDATO II KIDATO III KIDATO IV MAZOEZI

UTANGULIZI

Kiswahili ni somo la lazima katika shule za msingi na upili. Hii ni kutokana na dhima na umuhimu wake hapa nchini Kenya. Hii ndiyo lugha ya taifa letu. Imetambulika kuwa na uwezo wa kuleta umoja wa kitaifa. Fauka ya haya, Kiswahili si lugha ya tabaka au kabila moja. Ni lugha ambayo kila mtu wa kila kabila na rika katika taifa zima anaweza akadai kuwa ni yake.

Kiswahili kinachangia ujenzi wa taifa. Taifa linahitaji maarifa ya kuchambua na kuelewa nyenzo za kudumisha jamii na kuyatawala mazingira. Lugha ya Kiswahili inafaa sana kupitishia maarifa, dhana na stadi hizi.

Lugha inafungamana na utamaduni wa jamii na inapata maudhui na maana kutokana na hadhi ya maisha ya watu. Kwa hivyo, ni chombo kinachoweza kueleza mapokeo na itikadi za jamii fulani. Kama lugha ya Kiafrika, kufundishwa kwa Kiswahili kunadhihirisha vipengele fulani vya utamaduni wa mwafrika. Kwa mfano, kupitia kwa fasihi andishi na fasihi simulizi, somo la Kiswahili linatumika kumwelekeza mwanafunzi kuhakiki mambo iii kuchukia m na kuzingatia yale yanayoambatana na misingi ya taifa bora.

Ni fahari kuu kuona kuwa Kiswahili ni lugha ya taifa Tanzania na Kenya. Imeonyesha cheche za udhihirisho kuwa imesaidia sana katika kueneza maendeleo ya siasa, elimu, utamaduni na mambo mengine muhimu baina ya Kenya na mataifa mengine. Kwacho, watu wanabadilishana mawazo, jambo ambalo ni msingi wa maingiliano, uelewano na ushirikiano hasa katika enzi hizi ambapo mataifa mbalimbali yanaungana pamoja iii kurahisisha maingiliano kibiashara, kijamii, kiutamaduni na kadhalika.

Mafunzo ya lugha, hasa mitindo na sajili mbalimbali yatamwadabisha mwanafunzi kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili kutegemea miktadha, kaida na miiko katika jamii za kiafrika. Hili ni muhimu kwani imekadiriwa kuwa lugha ya Kiswahili inazungumzwa na mamilioni ya wakazi wa mataifa mbalimbali ya Afrika, licha ya mengine yaliyo nje ya bara Ia Afrika.

Kwa hivyo pana haja ya kutoa mafunzo kabambe yatákayomwezesha mwanafunzi kuwa na umilisi wa kutumia Kiswahili katika shughuli za kila siku. Jambo hili ni muhimu zaidi tukizingatia kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya pili kwa wengi wa wakenya. Halikadhalika, inakabiliwa na maingiliano ya lugha na vilugha vinginevyo. Kama lugha ya pili, inahitaji kutolewa mwongozo mzuri wa mafunzo.

Mafunzo katika silabasi hii yamegawanywa katika sehemu nne kulingana na stadi nne za

kujifunza lugha pamoja na sarufi na matumizi ya lugha. Nazo ni:

a)      Kusikiliza na kuzungumza

b)      Sarufi na matumizi ya lugha

c)      Kusoma

d)      Kuandika

Sehemu hizi zimetengwa kutegemea umilisi mahususi wa kimawasiliano ambao

mwanafunzi anatarajiwa kuupata kufikia mwisho wa elimu ya kiwango cha sekondari. 

Kusikiliza na kuzungumza

Kusikiliza na kuzungumza ni stadi za kimsingi na muhimu sana katika kujenga haiba ya mwauafunzi, uwezo wake wa kuwasiliana, kuhusiana na watu wengine na kujiendeleza kielithu. Pia stadi hizi huchangia kuimarisha stadi za kusoma na kuandika. Umilisi wa stadi hizi hutegemea kama mwalimu anatumia muda mwingi kumshirikisha mwanafunzi katika shughuli za kimtagusano (kimaingiliano) kama vile mazungumzo, dayolojia, michezo y Iugha na mijadala kwenye miktadha na mazingira yanayoakisi hali halisi. Fasihi an na simulizi zitatoa miktadha ya kuimarisha ustadi wa kusikiliza na kwzungumza.

Sarufi na matumizi ya lugha

Sarufi ndiyo nguzo ya lugha. Ni utaratibu wa kanuni zinazotawala matumizi sahihi ya viambishi vya maneno na sentensi kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe. Mwanafunzi atahitaji kuelekezwa kuhusu jinsi ya kuchanganua, kufafanua na kuunganisha viambishi, maneno na sentensi iii kutoa na kupokea maana halisi katika matumizi na miktadha mahususi ya kimazungumzo na kimaandishi kutegemea mahitaji, mahusiano, mazingira na kaida zajamii.

Kusoma

Stadi hii ni muhimu katika maisha ya kila siku ya mwanafunzi darasani, shuleni na ulimwengu wa nje. Mwanafunzi asome maandishi ya kawaida, kiuamilifu na kisanii huku akipewa mshaw wa kumudu na kufurahia miundo ya sentensi, msamiati na istilahi kwa kuihusisha na tajriba na vile vile mazingira yake. Ufundishaji wa stadi hii yapasa ulenge kumhusisha mwanafunzi katika utendaji kikamilifu.

Kuandika

Kuandika ni stadi ngumu làkini ya kikati katika maisha ya kisasa. Umuhimu wake unabainika katika mawasiliano, kunukuu, kuweka kumbukumbu na kujibu maswali ya mitihani. Stadi hii huchangia na pia hutegemea kuimarishwa kwa stadi zingine. Yapasa mwanafunzi atayarishiwe kazi za utungaji wa kawaida, kiubunifu, kiuamilifu na kisanii lakinibaada ya kuzisikiliza, kuzizungumzia na kuzisoma kikamilifu. Kwa nainna hii, mwanafunzi ataweza kubuni, kuchambua, kuhakiki na kuandika mambo mbalimbali yenye mantiki na mtiririko wa mawazo iwa kuzingatia kanuni za utungaji ipasavyo. Uandishi wa mikusanyo ya fasihi simulizi na tahakiki zake utachangia mno uimarishaji wa stadi hii.

Kufananisha mafunzo

Katika kidato cha kwanza na cha pili, mwalimu ana vipindi vitano vya kufundisha lugha. Katika kidato cha tatu na nne ana vipindi sita. Iii kuitumia silabasi hii kwa ufanisi, mwaliinU anashaunwa kuzingatia mambo yafuatayo:

  1. Math za silabasi liii zimepangwa kulingana na vidato. Inapendekezwa math hizi zifunzwe kwa njia ya kuchanganya na si kwa kufuata mfuatilizo wa math uliomo kwenye silabasi. Kwa miano, katika Inina moja katika kidato cha tatu, mwalimu anaweza kuteua math za kufundisha ifuatavyo:

(a)                Kusoma kwa ufahamu;

(b)               Sarufi na matumizi ya lugha;

(c)                Kuandika kiuamilifu;

(d)               Kusoma kwa kina k.m. tamthilia teule;

e) Kusoma kwa mapana ambapo atachagua majarida au maandishi yenye maswala ibuka kama vile Ukimwi, mazingira n.k.

f) Kusikiliza na kudadisi (k.m. fasihi simulizi - visasili).

2. Shabaha zilizoorodheshwa ni za kumwongoza mwalimu. Anashauriwa azitumie kuzua shabaha mahususi za kufundishia darasani.

Mwalimu afundishe kwa mwelekeo mseto. Haya yatekelezwe kwa ngazi mbili ifuatavyo:

a)      Mwalimu anapofundisha somo kama vile sarufi, ajaribu kujumuisha stadi zingine za lugha katika kipindi hichohicho.

b)      Masomo ya lugha na fasihi yachangiane. Yaani mwanafunzi anapozingatia fasihi aturnie matini ya fasihi kama muktadha wa kufafanua vipengele vya sarufi, msamiati, istilahi n.k.

3. Mwalimu atilie mkazo uwezo wa kuwasiliana kwa kuzingatia stadi za lugha. Ni muhimu mwalimu azue njia na kubuni vifaa vingi vya kufundishia kutegemea uwezo, mahitaji na mazingira ya mwanafunzi. Lengo la mwalimu liwe kumpa mwanafunzi nafasi ya kutagusana (kuingiliana) na wengine, mwalimu, waalikwa, matini na mazingira.

4. Silabasi haiorodheshi msamiati kama mada ya kujisimamia. Mwalimu anatarajiwa kufundisha msamiati na istilahi kimuktadha. Mwalimu ajitahidi kutafuta na kupanua msamiati na istilahi mpya kila zinapozuka kutokana na matini za fasihi, ufahamu, magazeti n.k. Baadhi ya maneno ya kumwelekeza mwanafunzi kujifunza ni msamiati wa kiteknolojia, maumbo, akisami, sehemu za mwili n.k.

5. Maarifa na lugha ni nyanja zinazotanzuka kila siku. Mwalimu awe macho daima ili kutambua mambo mapya na maswala yanayoibuka katika jamii na kuyajumuisha katika ufundishaji wake.