Search this site or the web

Site search Web search

KIDATO I KIDATO II KIDATO III KIDATO IV MAZOEZI

MADHUMUNI YA KUFUNIMSHA KISWAHILI KATIKA SHULE ZA UPILI

Mafunzo yanayotolewa kwa mwanafunzi katika shule za upili kwa muda wa miaka minne yanatarajiwa:

1.  kuendeleza mafunzo ya Kiswahili yaliyoshughulikiwa katika shule za msingi

2.  kumpa uwezo wa kudumu wa kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika ipasavyo kwa lugha ya Kiswahili

3. kumwezesha kubuni, kuchambua na kujieleza wazi na kimantiki

4.kutumia Kiswahili katika mawasiliano na shughuli za kila siku

5. kutambua, kudadisi, kuthamini na kustawisha ama na tanzu mbalimbali za lugha na fasihi kwa Kiswahili

6. kujifunza na kuthamini fani mbalimbali za tamaduni kwa kutumia Kiswahili

7.  kuwa na utambuzi kwa mambo yanayohusu na yanayoiathiri jamii k.m. Ukimwi, maendeleo ya kiteknolojia, usawa wa kijinsia n.k.

8.   kuhifadhi mazingira kwa ajili ya kudumisha uhai na kujitimizia mahitaji ya kila siku na ya maisha ya baadaye

9.  kufurahia kujisomea na kujiendeleza mwenyewe kadiri ya uwezo wake

10.  kuthamini, kufurahia na kujivunia Kiswahili kama lugha ya taifa na kimataifa.