Search this site or the web

Site search Web search

1.0.0 KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

1.0 Shabaha

Kufikia mwisho wa kidato cha kwanza, mwanafimzi aweze:

a)      kuzingatia matamshi bora ya lugha ya Kiswahili.

b)      kutambua na kurekebisha athari zitokanazo na lugha za mama na lugha nyinginezo.

c)      kustawisha mawasiliano yafaayo kulingana na kaida za jamli.

d)      kukuza kiwango cha msamiati kwa ajili ya mawasiliano mbalimba

e)      kufurahia na kuzungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.

f)        kubuni na kujieleza kikamilifu.

g)      kufurahia tanzu mbalimbali za fasihi.

h)      kuzinlatia mafunzo na maadili yanayojitokeza katika kazi mbalimbali.

i)        kukuza uwezo wa kukusanya na kuhifadhi kazi za fasihi simulizi.

j)        kukuza utendaji wa kisanii.

 

1.2 Yaliyomo

1.2.1 Matamshi bora

a)      Kiimbo

b)      Shadda

c)      Irabu/vokali - /a /e/, ui, /0/, /u!.

d)      Konsonanti - /b/ch/, /d, /dh/,/f/, /g/,/gh/, /h/, /j/, /k/, ill, Im!, In!, /ng’/, /ny/, /p/, /r/, /s/, /sh/, /t’, /th/, /v/, /w!, /y/,/z/

e)      Ala za sautilkutamkia

f)        Namna ya kutanika na ama za sauti k.m. ghuna,sighuna/hafifii,vipasuo,

vikwamizo n.k.

g)      Silabi

h)      Maneno

i)        Vitate k.m. baba, papa

j)        Vitanza ndimi

1.2.2 Maamkizi na mazungumzo

a)      Maamkizi na mazungumzo ya:

i)                    Nyumbani

ii)                   Dukani

iii)                 Mtaani

iv)                 Sokoni

v)                  Shuleni

b)      Mahojiano k.m. mwalimu na Mwanafunzi

c)      Mijadala k.m. umoja na utangamano katika familia

d)      Hotuba

 

1.2.3 Ufahamu wa kusikiliza

Ufahamu wa taarifa za kusikiliza

1.2.4 Kusikiliza na kudadisi

a)      Utangulizi wa fasihi

i)                    Maana

ii)                   Aina

b)      Fasihi simulizi

Vipera vya fasihi simulizi

i) Hadithi - utambaji

-         hurafa

-         hekaya

ii) Semi

-         Methali

-         Vitendawili, mafumbo na chemsha bongo

-         Misemo

iii) Ushairi

-         Nyimbo

c)      Maigizo: yategemee shabaha na muktadha k.m. jandoni, sherehe za arusi n.k.

 

Shughuli hizi zizingatie:

Matamshi bora, sarufi, msamiati, lugha na tamathali za semi, mafunzo na maadili na maswala ibuka k.m. teknolojia, tarakilishi/kompyuta, afya, na Ukimwi, mazingira, haki za watoto na za kibinadamu n.k.

 

Mapendekezo

Kutokana na umuhimu wa stadi hizi, mwalimu amshirikishe mwanafunzi katika shughuli zitakazochangia uwezo wake wa matamshi bora, kurekebisha makosa, mawasiliano na utendaji wa kazi za kisanii. Hili litawezekana iwapo mwalimu atachagua njia na vifaa vya kufundishia kutegemea uwezo, mahitaji na mazingira ya mwanafunzi. Mwalimu anahimizwa kuwa mbunifu katika kutekeleza haya. Mwalimu awahusishe wanafunzi katika matamshi bora, matumizi ya lugha ya adabu, utafiti na kuki matini za fasihi simulizi.

Mwalimu atumie vifaa kama vinasa sauti, mafanani, waalikwa na wanafunzi wenyewe kuzua mada za kusikiliza na kuzungumza.

Tathmini ifanywe kupitia maswali .ya ufahamu, kuchunguza utendaji wa wanafunzi, kazi mradi, n.k.